Date: 
21-06-2023
Reading: 
Warumi 12:1-2

Jumatano asubuhi tarehe 21.06.2023

Warumi 12:1-2

1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Mungu hutunza Kanisa lake;

Mtume Paulo anawasihi Warumi kuitoa miili yao iwe dhabihu iliyo hai, takatifu ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenye maana. Anawataka wasifuatishe mambo ya dunia, bali wageuzwe nia zao wakimpendeza Mungu katika ukamilifu.

Kuitoa miili kama dhabihu kwa ajili ya Bwana ni kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii pasipo kuchoka. Tunapoifanya kazi, yaani kumtumikia Mungu, mstari wa kwanza unasema tunaifanya ibada yenye maana. Ibada yenye maana ni kuishi kwa kadri ya mapenzi ya Mungu, ili tudumu katika utunzaji wa Mungu. Amina.

Siku njema.

Heri Buberwa