MATANGAZO YA USHARIKA 

 TAREHE 11 JUNI, 2023

NENO LINALOTUONGOZA NI

MUNGU AU ULIMWENGU 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 04/06/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.  

5. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia Washarika wenye Watoto wa Kipaimara mwaka wa pili kuwa kutakuwa na mtihani ngazi ya kwanza ya Dayosisi tarehe 25/06/2023. Hivyo wazazi mnaombwa kusaidia kuwahimiza Watoto kuhudhuria mafundisho kwa muda uliopangwa.

6. Uongozi wa umoja wa vijana unapenda kuwatangazia vijana wote kuwa siku ya jumatano saa kumi na moja jioni kutakuwa na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya vijana. Vijana wote mnakaribishwa. Pia vijana wameandaa Tshirt ambazo zitauzwa hapo nje. Washarika mnaombwa kuwaunga mkono.

7. Kwaya ya Umoja itaendelea na mazoezi ya reformation siku ya Jumatatu saa 11.00 jioni. Waimbaji wote mnaombwa kuhudhuria.

8. SHUKRANI – TAREHE 18/06/2023 KATIKA IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI

Familia ya Marehemu Rabian na Nsia Kimaro watamshukuru Mungu kwa kuendelea kuwafariji, kuwalinda, kimaisha na kuwapigania tangu Baba yao mpendwa Mzee Rabian Elia Kimaro alipotwaliwa na Bwana.

Neno: Isaya 41:10, Wimbo: TMW 49 (Nakutegemea Yesu)

9. Ratiba ya Kambi ya watoto Azania Front Cathedra Tarehe 14 -15 Juni 2023

Jumatano Tarehe 14/06/2023 

  • saa 4-6 asubuhi ---- AFYA, MAZINGIRA NA UKUAJI 
  •  
  • saa 7:30-9:30 mchana ---- MTOTO NA UTANDAWAZI 

Alhamisi Tarehe 15/06/2023 

  • saa 4-6 mchana ---- UPENDO NA MSAMAHA 
  •  
  • saa 7:30-9:30 mchana ---- HAKI NA WAJIBU WA MTOTO, UNYANYASAJI WA MTOTO NA JINSI YA KUJIKINGA   

WATOTO WAFIKE SAA 2 NA NUSU ASUBUHI WAKIWA WAMEKWISHA KUNYWA CHAI NYUMBANI. WATAPATA CHAKULA CHA MCHANA KANISANI. Watarejea nyumbani saa 9:30 mchana

10. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 24/06/2023

SAA 10.00 JIONI

  • Bw. Albert Ernest Swai na Bi. Grace John Msangi

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana na Bibi Desmond Mushi
  •  
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:  Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
  •  
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki 
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr. Abedi na Eng. Elisifa Kinasha
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Happines Nkya
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Eng. Na Bibi Harold Temu
  •  
  • Tabata: Kwa Mchungaji Kibona
  • English Service: kwa Dr Mpale Silkiluwasha Chuo Kikuu UDSM

12. Zamu: Zamu za wazeeni Kundi la Kwanza

13. Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.