MATANGAZO YA USHARIKA 

 LEO TAREHE 04 JUNI, 2023

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI MUNGU BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.

3. Matoleo ya Tarehe 28/05/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.  

5. Jumapili ijayo tarehe 11/06/2023 ni siku ya Ubatizo wa Watoto na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

6. Leo tarehe 04/06/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika Karibuni.

7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia Washarika wenye Watoto wa Kipaimara mwaka wa pili kuwa kutakuwa na mtihani ngazi ya kwanza ya Dayosisi tarehe 25/06/2023. Hivyo wazazi mnaombwa kusaidia kuwahimiza Watoto kuhudhuria mafundisho kwa muda uliopangwa.

8. Uongozi wa umoja wa vijana unapenda kuwatangazia vijana wote kuwa siku ya jumatano saa kumi na moja jioni kutakuwa na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya vijana. Vijana wote mnakaribisha

9. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 11/06/2023 

IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI

  • Familia ya Dr Samuel na Jennifer Swai watamtolea Mungu sadaka ya shukrani kwa mambo mengi aliyowatendea, kumlinda na kumtunza Mama yao Apaisaria P. Swai kufikisha umri wa miaka 95 mnamo tarehe 02.06.2023 kuwalinda watoto wao shuleni na Dr Swai kuhitimisha utumishi wake umma.

Neno: 1 Nyakati 16:8, Wimbo: TMW 262- Tumshukuru Mungu.

 IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI

  • Mama Erica Byatato Pamoja na familia watamshukuru Mungu kwa kumlinda salama Ma Erica na kumfikisha miaka 80. 

Neno: Zaburi ya 103:1-2, Wimbo wa Kwaya Kuu: Namba 518 - Chini ya Mbawa Zako, Ee Yesu nifiche.

  • Family ya David Mwalusamba inapenda kumshukuru Mungu kwa kumaliza salama msiba wa mpendwa/mama yao mpenzi pia kumsafirisha kwenda Mbeya kyela na kumpumzishana wamerudi salama

Neno: Wimbo: Namshukuru Mungu toka kwaya ya vijana na Bwana Yesu ni ngome yangu toka kwaya kuu

  • Kikundi cha maigizo watamshukuru Mungu kwa kuwapigania tangu kuanzishwa kwa kikundi hiki, kuendelea kuwaongoza katika mikakati wanayopanga Pamoja na kuwasaidia kutimiza malengo waliyojiwekea katika kipindi hiki cha miezi sita.

Neno: Zaburi 150 

10. Uongozi wa usharika unapenda kuwatangazia wazazi wa watoto wa shule ya jumapili kuwa tarehe 14-15/06/2023 kutakuwa na kambi ya watoto hapa usharikani muda ni saa 02.30 asubuhi hadi 10:00 jioni masomo yatakayofundishwa ni

  • Afya, mazingira na ukuaji
  • Haki za watoto , wajibu wa watoto
  • Kufahamu na kupinga ukatili
  • Upendo na msamaha
  • Watoto na utandawazi

Na tarehe 17.06.2023 watakwenda usharika wa kitunda relini kuhitimisha mafunzo hayo katika ngazi ya jimbo, kwaajili hiyo tunaomba ushirirkiano wenu wazazi na kuwahimiza watoto kuja kujifunza.

11. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

SAA 10.00 JIONI

Bw. Albert Ernest Swai na Bi. Grace John Msangi

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

 

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana Towo
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:  

         Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo

  • Kinondoni: Kwa Prof. na Bibi S. Kulaba 
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Yono Kevela
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Dr. na Bibi Rumishael Shoo
  • Tabata: Kwa Mchungaji Kibona

 

13. Zamu: Zamu za wazeeni Kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.