Date: 
16-05-2023
Reading: 
1Yohana 3:19-24

Hii ni Pasaka 

Jumanne asubuhi tarehe 16.05.2023

1 Yohana 3:19-24

19 Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake,

20 ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.

21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;

22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.

23 Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.

24 Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.

Ombeni katika jina la Yesu;

Mungu ni mkuu aliye juu ya vyote. Aliufanya uumbaji wa dunia na vyote vilivyomo, hivyo nasi tu mali yake. Ndiyo maana Yohana anaandika kuwa tunatakiwa kumuomba yeye tukizishika amri zake. Yohana anaonesha kuwa tukimwamini Yesu na kupendana, yeye hukaa kwetu, husikiliza sala zetu.

Tunachokiona katika somo la asubuhi hii ni nafasi ya Mungu kwetu, kama Baba aliye Muumbaji wa vitu vyote. Yeye ni Mkuu aliye juu ya vyote. Nafasi hii inatosha kabisa kutukumbusha kuwa tuishi kwa kumuomba yeye tu, maana ndiye atuongozaye siku zote na kutupa haja zetu. Tumuombe kwa Imani, kwa jina la Yesu. 

Jumanne njema.

 

Heri Buberwa