Katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral, 7 Aprili 2023 na kuongozwa na Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa iliwakutanisha washarika na wageni mbalimbali kukumbuka siku ambayo Yesu Kristo aliteswa na kufa pale msalabani kabla ya kufufuka siku ya tatu.
Akizungumza katika utangulizi wa ibada hiyo Baba Askofu alisema kuwa Ijumaa Kuu ni siku ambayo Mwokozi Yesu Kristo alihukumiwa katika kesi ya ajabu ambayo ilikuwa imetengenezwa na viongozi ambao walimwona kama analeta dini mpya yenye kukusudia kuwapindua kutoka mamlakani, “Mungu anaweza kukupa madaraka ukashindwa kuyatumia, Pilato ni mfano mzuri sana maana alikuwa na madaraka lakini alikosa mamlaka ya kuwaambia hapana wale waliomleta Yesu kwake wakidai asurubiwe. Pilato alifikiri kwa kunawa mikono basi atakuwa amejiondolea hatia”. Baba Askofu alidokeza.
Somo: Aliteswa na Kufa Kwa Ajili Yetu; Marko 15: 21 - 37
Baba Askofu alisema kwa sasa si wakati wa mkristo kumtafuta mtu akuombe kila muda, kwa sababu pazia la hekalu limepasuka, hivyo kila mtu anaweza kwenda na kuzungumza na Yesu moja kwa moja na akamsikia. Alihimiza pia kutokuwa watu wakutaka kuombewa na watu kila wakati. Pia alisema yatupasa kuwa mawakili wazuri wa Yesu Kristo iwe nyumbani au popote pale ambapo Mungu amekuweka.
Ibada ya tatu ya Ijumaa kuu iliambatana na igizo la Pasaka kuelezea kile alichopitia Yesu kuanzia kukamatwa kwake mpaka kufa kwake Msalabani.
Ibada za Ijumaa Kuu kwa lugha ya Kingereza na Kijerumani ziliongozwa na Mchungaji Joseph Mlaki akiwa pamoja na Mchungaji Anne Mika.
PICHA KUTOKA KATIKA IBADA ZA IJUMAA KUU;
Kutazama ibada za Ijumaa Kuu:
Ibada ya Kwanza - Kiswahili: https://www.youtube.com/watch?v=P_DEKp-x0Hc
Ibada ya Pili - Kiingereza/ Kijerumani: https://www.youtube.com/watch?v=5FLtw9SWreg
Ibada ya Tatu - Kiswahili na Igizo la Pasaka: https://www.youtube.com/watch?v=WhAXZzguGN8&t=6535s