Date: 
05-05-2023
Reading: 
2 Wakorintho 4:6-18

Hii ni Pasaka;

Ijumaa asubuhi tarehe 05.05.2023

2 Wakorintho 4:16-18

16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.

17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;

18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.

Maisha mapya ndani ya Yesu;

Mtume Paulo anaongelea juu ya kutolegea katika Kristo na kudumu katika Imani kwa upya kila siku. Kwa mujibu wa Paulo, dhiki haina nafasi katika maisha aaminiye. Haimaanishi kuwa hatuwezi kukutana ma dhiki, bali katika dhiki tumaini letu ni Kristo. Paulo anaelekeza kuviangalia visivyoonekana, yaani tuwe na Imani katika Kristo.

Msingi wa ujumbe wa Paulo ni kudumu katika Imani katika Kristo ambayo hutufanya wapya kila siku. Imani hiyo inakuwa thabiti tukilisoma na kulishika neno la Mungu, kwa matendo mema. Haya ndiyo maisha mapya ndani ya Yesu.

Siku njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri