MATANGAZO YA USHARIKA 

LEO TAREHE 30 APRILI, 2023  

NENO LINALOTUONGOZA WIKI HII NI

MAISHA MAPYA NDANI YA YESU  

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 23/04/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwa kumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. SHUKRANI – Jumapili ijayo tarehe 07/05/2023 – Ibada ya kwanza saa 1.00 asubuhi.

Dada Irene David atamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomtendea, Siku ya kuzaliwa 06/05/1994, kumtia nguvu na kumtunza tangu Mama yake mzazi alipotwaliwa na Bwana tarehe 06/05/2004 pia kumaliza matibabu salama tangu agundulike na Brest Cancer miaka mitano iliyopita.

Neno: Zaburi 23, Wimbo: TMW 398

6. NDOA. HAKUNA NDOA ZA WASHARIKA

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

7. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:  

Kwa Dr. na Dr. Matee 

- Mjini kati: Watatangaziana  

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki  

- Upanga: Kwa Mama Suzan Mboya

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach:Kwa Bwana na Bibi Godfrey Monyo

- Tabata: Kwa Mchungaji Kibona

- English Service: Watatangaziana

8. MAHUDHURIO IBADA YA JUMAPILI ILIYOPITA 23/04/2023

JUMLA IBADA ZOTE WATU WAZIMA NI 514

SHULE YA JUMAPILI 106

9. Zamu za wazeeni Kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.