MATANGAZO YA USHARIKA 

LEO TAREHE 23 APRILI, 2023  

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

 YESU KRISTO NI MCHUNGAJI MWEMA 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 16/04/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwa kumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Uongozi wa shule ya jumapili unawaomba wazazi kuwaleta Watoto siku ya jumamosi saa 7.00 mchana kwaajili ya mazoezi ya maandalizi ya Tamasha la uimbaji ngazi ya jimbo.

6. Kwaya ya Umoja itaanza mazoezi siku ya jumanne saa 11.00 jioni. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria mazoezi haya kwa ajili ya maandalizi ya uimbaji wa Kantate.

7. Kamati ya Malezi inaomba kukutana hapo nje kwenye jukwaa na wazazi wa Watoto wa Sunday School Pamoja na Kipaimara mara baada ya ibada hii kwa muda mfupi sana. Mungu awabariki kwa utayari wenu.

8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 29/04/2023.

SAA 08.00 MCHANA

Bw. Ramon Karim Nawab na Bi. Lulu Nancy Ishengoma

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:  Kwa Mzee Evatt Kuzilwa  
  • Mjini kati: Ibada itakuwa kanisani
  • Kinondoni: Kwa Dr. na Bibi T. Onesmo  
  • Upanga: Kwa Bibi Violet Maro
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: itafanyika siku ya Jumatano saa 11 jioni kwa Bwana na Bibi Zebadiah Moshi.
  • Tabata: Kwa Mchungaji Kibona

10. MAHUDHURIO IBADA YA JUMAPILI ILIYOPITA 09/04/2023

JUMLA IBADA ZOTE WATU WAZIMA NI 669

SHULE YA JUMAPILI 183

11. Zamu: Zamu za wazeeni Kundi la Pili.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.