Ni siku maalumu iliyokuwa inangojwa kwa hamu kubwa na ya kipekee kwa Kwaya Kuu ya Azania Front, ni tarehe 7 Septemba
2014 ya kuzindua mkanda wao vol. ya tisa (9). Kikundi kiliingia kanisani asubuhi kikiongozwa na Mwalimu mzoefu na wa siku
nyingi Abisai Faragha mpiga kinanda na mfundishaji wa nyimbo za noten au nyimbo sanifu, Kwaya ilingia Ibada ya kwanza,
na hatimaye Ibada ya pili na kuanza uimbaji moja kwa moja kutegemea na liturgia iliyokuwa ikiongozwa na Mchungaji Kiongozi
-Chaplain Charles Mzinga.
Kanda ilizinduliwa katika Ibada zote na iliambatana na maombi maalumu ya kuiombea kwaya ili kanda iweze kuleta utukufu
hata kwa msikilizaji. Kwaya ilifanya vizuri na ilileta msisimko mkubwa sana, na katika nyimbo mbili zilizoimbwa watu
walizipokea vizuri na haikuwa kazi kubwa hata kwa Mchungaji alipoita watu kuja kununua au kuchangia kwaya kwenda mbele
kutoa bila matatizo. Na hii ndio Risala iliyotangulia kusomwa na Mlezi wa Kwaya Kuu Mama Elipina Mlaki ambaye sasa ni
Mzee wa Kanisa. Alisoma kwa makini na weledi wa hali ya juu. Bofya hapa kusoma risala....
Kwaya Kuu imepokea vingozi wapya wa kikundi mwaka huu baada ya uchaguzi 2014 ambao ni
-Â - Elisha Mushumbusi - Mwenyekiti
-Â - Suzan Muro Towo - Makamu Mwenyekiti
-Â - Grace Makalla - Katibu
-Â - Margreth Godwin - Katibu Msaidizi
-Â-- Heri Nteboya - Mtunza Hazina
-Â-- Edward Mkony - Mtunza Hazina Msaidizi
-Â - Mwl Abisai Faragha - Mwalimu Mkuu wa kwaya
Tunamshukuru Mungu kwa ajili yao na tunawaombea kwa Mungu wasichoke njiani na waweze kuifanya kazi ya Mungu kwa
uaminifu na mafanikio injili isonge mbele.
Jumuisho
Mwalimu, Viongozi na wanakwaya kwa ujumla wanapenda kuwashukuru watu wote kwa ushirikiano mzuri waliouonyesha
kipindi chote cha maandalizi na kufanikisha zoezi zima la Uzinduzi. Na wale waliotoa mali zao Muda wao na yote.
MUNGU WETU ALIYE HAI AWABARIKI SANA.
Mmoja wa walezi wa Kwaya Kuu Mama E. Mlaki akitoa maelezo mafupi kwa washarika siku ya uzinduzi wa mkanda Vo. 9 kwa niaba ya
wanakwaya kuu na walezi Tar 7 Septemba 2014.
Kwaya Kuu wakiwa katika Ibada siku ya uzinduzi wa kanda Vo. 9 Tarehe 7 September 2014
Kwaya kuu wakionesha na kuimba siku ya uzinduzi katika ibada wakiongozwa na Mwl Abisai Faragha.
Wanakwaya Kuu Azania Front wakiimba wakati wa Ibada siku ya uzinduzi.
Doscar Vuhahula na Mama Anna Kavugha wakiwa katika uimbaji siku ya uzinduzi.
Isabela Hingi na Doscar Vuhahula wakiwa katika uimbaji siku ya uzinduzi.
Mwl Abisai Faragha akiongoza kwaya wakati wa ibada siku ya uzinduzi
Mchungaji Charles Mzinga akifanya maombi baada ya wanakwaya kuimba siku ya uzinduzi Azania Front na kubariki kanda vo. 9.
Mzee Buchanagandi (Mzee wa kanisa)akichangia kwa kununua kanda siku ya uzinduzi.
ÂÂ
Mzee Minja wa kwaya ya Upendo Azania Front akimnunulia mke wake kanda siku ya uzinduzi.
Mzee George Mnyitafu, mmoja wa walezi wa Kwaya akinunua kanda siku ya uzinduzi.
Baadhi ya waimbaji wakichangia kwaya yao kwa kununua kanda Doscar Vuhahula na anayefuata Mama Omega Mongi.
Mama E. Mlaki Mlezi wa kwaya Kuuu akinunua kanda siku ya uzinduzi.
Kwaya kuu Azania Front wakiwamalizia ibada nje baada ya uzinduzi.
Mwenyekit i wa Kwaya Kuu Azania Front Bw. Elisha Mushumbusi akisalimiana na mmoja wa walezi wa kwaya Kuu Mzee Benjamin Mpamo
baada ya ibada ya Uzinduzi.
Kutoka kushoto Ni mama Anna Kavugha, Erica Byabato na Waeli R. Koshuma waimbaji wa muda mrefu katika kwaya kuu ya Azania Front.
Mama Anna ameimba kwa miaka 54 mpaka sasa na Mama Waeli ameimba kwa Miaka 58 mpaka sasa!
Baada ya uzinduzi viongozi wa kwaya Kuu wakihesabu walichokusanya siku ya uzinduzi.
Mmoja wa washarika wa Azania Front Mzee Kida akichangia kwa kununua kanda ya kwaya siku ya uzinduzi 7 septemba 2014 akisindikizwa na
Mama C. Nzali mwimbaji kwaya kuu.
Mzee Adam Mpanda mmoja wa wanakwaya kuu akinunua kanda ya kwaya kuu siku ya uzinduzi.
Mama Waeli Koshuma Kushoto na Mama Anna Kavugha Kulia wakiombewa na Mch C. Mzinga baada ya kutoa shukrani ya pekee kwa jinsi Mungu
alivyowajalia kumtumikia kwa njia ya uimbaji tangu wakiwa wasichana mpaka leo. Mama Anna kwa Miaka 54 na Mama Waeli kwa mika 58.
Pembeni ni Mwenyekiti wa kwaya kuu akushuhudia tendo hilo.