Date: 
07-12-2022
Reading: 
Warumi 15:7-13

Hii ni Advent 

Jumatano asubuhi tarehe 07.12.2022

Warumi 15:7-13

7 Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe.

8 Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;

9 tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.

10 Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na watu wake.

11 Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana; Enyi watu wote,mhimidini.

12 Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Bwana anakuja tuandae mioyo yetu;

Mtume Paulo anawaandikia Warumi kuishi katika umoja wa Kikristo ili Mungu atukuzwe katika Taifa lake. Katika umoja huo, Paulo anawahimiza kudumu katika ibada na tafakari wakimshukuru Mungu. Paulo anarejea utabiri wa kuzaliwa kwa Yesu kama ulivyotolewa naye nabii Isaya, akimtaja huyu Yesu kama tumaini la ulimwengu.

Yesu huyu anayetajwa na Mtume Paulo ndiye tunaelekezwa nasi kumwabudu na kumtumaini katika njia zetu. Tunaalikwa kukaa katika umoja wa Kikristo tukimwabudu na kutengeneza maisha yetu, ili atakaporudi tuurithi uzima wa milele.

Siku njema