Ijumaa asubuhi tarehe 25.11.2022
Ufunuo wa Yohana 11:7-13
[7]Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.
[8]Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa.
[9]Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini.
[10]Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.
[11]Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.
[12]Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.
[13]Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.
Uzima wa ulimwengu ujao;
Yohana alifunuliwa juu ya watu wakaao juu ya nchi wakifurahi katika Bwana baada ya kupitia shida na mateso mengi. Sauti kutoka mbinguni inawaita kutoka katika mateso ya adui zao, ili waingie kwenye furaha ya milele. Ni wale waliomwamini Yesu, tayari kuingia katika uzima wa milele.
Furaha ya milele ipo kwa ajili yetu. Ni wajibu wetu kutumia nafasi yetu vizuri kama tulivyompokea Yesu, tukidumu katika Imani timilifu. Imani ya kweli yenye matendo ndiyo kigezo cha kuurithi uzima wa milele.
Siku njema.