Date: 
18-11-2022
Reading: 
Isaya 24:1-4

Ijumaa asubuhi tarehe 18.11.2022

Isaya 24:1-4

[1]Tazama, BWANA ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake.

[2]Na itakuwa kama ilivyo hali ya watu, ndivyo itakavyokuwa hali ya kuhani; kama ilivyo hali ya mtumwa, ndivyo itakavyokuwa hali ya bwana wake; kama ilivyo hali ya mjakazi, ndivyo itakavyokuwa hali ya bibi yake; kama ilivyo hali yake anunuaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake auzaye; kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake akopaye; kama ilivyo hali yake atwaaye faida, ndivyo itakavyokuwa hali yake ampaye faida.

[3]Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana BWANA amenena neno hilo.

[4]Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika.

Jiandae kwa hukumu ya mwisho;

Nabii Isaya anaelezea hukumu ijayo ya dunia kuwa Bwana ataipindua dunia na kuifanya ukiwa. Isaya anatoa picha ya kila mtu kuhukumiwa kwa kadri ya matendo yao, pasipo upendeleo. Mungu hapendi uovu ndiyo maana katika mstari wa tatu anaahidi kuiharibu dunia kabisa na kuifanya tupu.

Isaya alitabiri hukumu ijayo. 

Hukumu ijayo ipo, pale ambapo kila mmoja atahukumiwa mbele za Mungu. Maisha yako ni kielelezo cha hukumu utakayopewa na Bwana. Kumbe sisi wenyewe tunayo nafasi ya kujiandaa kwa hukumu, tukitenda mema maana tutahukumiwa kwa kadri ya matendo yetu. 

Siku njema.