Date: 
17-10-2022
Reading: 
1 Yohana 3:1-3

Jumatatu asubuhi tarehe 17.10.2022

1 Yohana 3:1-3

[1]Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.

[2]Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.

[3]Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.

Upendo wa kweli watoka kwa Mungu;

Yohana katika waraka wake anaandika kuwa sisi tulivyo ni kwa sababu ya pendo la Mungu, yaani tunaitwa wana wa Mungu kwa sababu ya pendo la Mungu. Yohana anaonesha kuwa tukiishi inavyotakiwa halafu wengine wasitutambue, ni kwa sababu hawajamtambua yeye aliyetupenda. Mkazo wa Yohana ni kwa waaminio kujitakasa na kudumu katika utakatifu, maana yeye aliyetupenda ni Mtakatifu.

Ujumbe wa asubuhi hii ni kufahamu kuwa kwa upendo wa Mungu tuko hivi tulivyo. Hivyo ni muhimu kuendelea kuishi maisha ya kumpa Mungu Utukufu maana tofauti na hapo ni kuukataa upendo wa Mungu. Mungu hajatupenda ili tuishi tunavyotaka, bali tumtumikie kwa uaminifu hata kufa ili atupe taji ya uzima. 

Tambua Mungu anakupenda

Umtumikie kwa furaha.

Uwe na wiki njema.