Jumamosi asubuhi tarehe 17.09.2022
1 Samweli 26:21-25
[21]Ndipo Sauli akasema, Nimekosa; rudi, Daudi, mwanangu; maana sitakudhuru tena, kwa kuwa maisha yangu yalikuwa na thamani machoni pako leo; angalia, nimetenda upumbavu, nimekosa sana.
[22]Daudi akajibu, akasema, Litazame fumo hili, Ee mfalme! Kijana mmoja na avukie huku, alitwae.
[23]Naye BWANA atamlipa kila mtu haki yake, na uaminifu wake; maana BWANA amekutia mikononi mwangu leo, nami nalikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi
wa BWANA.
[24]Tena, angalia, kama vile maisha yako yalivyokuwa na thamani machoni pangu, kadhalika na maisha yangu na yawe na thamani machoni pa BWANA, akaniokoe katika shida zote.
[25]Ndipo Sauli akamwambia Daudi, Ubarikiwe, Daudi, mwanangu; utatenda mambo makuu, tena hakika yako utashinda. Basi, Daudi akaenda zake; Sauli naye akarudi kwao.
Jirani yako ni nani?
Sauli alikuwa mtawala ambaye alitaka kumuua Daudi. Kuna wakati hakumpendeza Bwana, ilifikia hatua afe. Lakini pamoja na Daudi kuwa katika hatari ya kuuawa na Sauli, yeye hakuwa tayari kumuona Sauli akifa kama tunavyosoma hapa;
1 Samweli 26:8-9
8 Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hata nchi kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili. 9 Lakini Daudi akamwambia Abishai, Usimwangamize; kwani ni nani awezaye kuunyosha mkono wake juu ya masihiSauli hakuamini kilichotokea, kwamba Daudi ndiye alitaka asife! Daudi hakutaka kulipiza kisasi.
Tunakumbushwa kulipa jema kwa jema, baya kwa jema, yote kwa mema. Yesu alizuia kulipiza kisasi, maana ni sawa tu na wa mataifa! Ujirani mwema ni kutolipiza kisasi kwa jirani yako.
Jumamosi njema.