Date:
06-09-2022
Reading:
Kumbukumbu la Torati 23:21-23
Jumanne asubuhi 06.09.2022
Kumbukumbu la Torati 23:21-23
[21]Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.
[22]Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako.
[23]Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.
Tutumie vizuri ndimi zetu;
Mungu aliwaagiza Israeli kuhakikisha wanatimiza nadhiri zao. Aliwaelekeza kwamba kutotimiza nadhiri ilikuwa dhambi, hivyo walitakiwa kuepuka dhambi hiyo kwa kutimiza nadhiri zao. Kama wangeona wasingetimiza nadhiri husika, waliambiwa bora wasiweke nadhiri.
Nadhiri siyo jambo la kawaida kama ambavyo baadhi yetu tunaweza kuwa tunafikiria. Ukiweka nadhiri lazima uitimize. Usipoitimiza ni dhambi.
Kwa kuonesha umuhimu wa nadhiri, hata huku ulimwenguni huwa tunasema "ahadi ni deni". Sasa kama duniani tu ahadi ni deni, inakuwaje kama ukimuahidi Bwana (kuweka nadhiri) halafu usitimize? Timiza nadhiri yako (zako) kwa Bwana.
Siku njema.