Jumamosi asubuhi tarehe 23.07.2022
2 Wakorintho 2:12-17
[12]Basi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo, nikafunguliwa mlango katika Bwana,
[13]sikuona raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia.
[14]Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
[15]Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;
[16]katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo?
[17]Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.
Tunaitwa kuwa wanafunzi na wafuasi;
Mtume Paulo alipofika Troa alikosa raha kwa sababu hakumwona Tito ambaye wangekuwa wote. Lakini kwa sababu alimjua Mungu hakutetereka katika kazi yake. Paulo alizidi kunena neno la Kristo kwa ukamilifu wake, maana aliamini katika watu kuokolewa kwa jina la Kristo, na siyo kupotea.
Tunaitwa kuifanya kazi ya Mungu katika mazingira yoyote. Tusimtegemee mtu ili kazi ya Mungu iende mbele, bali tusaidiane na wenzetu kwa msaada wa Mungu. Tukisaidiwa na Mungu, hata kama tukiachwa na watu tunaowategemea, Mungu atatusaidia hata kwa kuwainua wengine.
Ujumbe mkuu ni kumfuata Yesu tukimtumikia kwa kumtegemea yeye.
Jumamosi njema.