IJUMAA TAREHE 1 OKTOBA 2021, ASUBUHI
1 Petro 2:1-5
1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
3 ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.
4 Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
Uchaguzi wa busara;
Asubuhi hii tunasoma juu ya kuweka mbali uovu na kuacha hila, unafiki na visingizio katika kumwamini Yesu Kristo. Yesu ni jiwe hai lililo teule, lililokubaliwa na Mungu.
Sisi ni mawe yaliyo hai, tuliojengwa kwa Roho katika Yesu. Hapa tuweke bidii ya kuendelea kuwa hai katika Kristo, kwa kuchagua kumtumikia BWANA, yeye aliye jiwe kuu, yaani Bwana na Mwokozi wetu kuelekea uzima wa milele.
Siku njema.
FRIDAY 1ST OCTOBER 2021, MORNING
1 Peter 2:1-5
1 Therefore, rid yourselves of all malice and all deceit, hypocrisy, envy, and slander of every kind. 2 Like new born babies, crave pure spiritual milk, so that by it you may grow up in your salvation, 3 now that you have tasted that the Lord is good.
The Living Stone and a Chosen People
4 As you come to him, the living Stone—rejected by humans but chosen by God and precious to him— 5 you also, like living stones, are being built into a spiritual house[a] to be a holy priesthood, offering spiritual sacrifices acceptable to God through Jesus Christ.
Footnotes
- 1 Peter 2:5 Or into a temple of the Spirit
Wise choices;
This morning we read about putting away evil and forsaking deceit, hypocrisy and excuses in believing in Jesus Christ. Jesus is the chosen, living stone approved by God.
We are living stones, built by the Spirit in Jesus. Here let us strive to continue living in Christ, by choosing to serve the LORD, the great rock, our Lord and Saviour, to eternal life.
Good day.