Date: 
08-07-2021
Reading: 
2 Timothy 3:10-17

THURSDAY 8TH JULY 2021,    MORNING                                               

2 Timothy 3:10-17 New International Version (NIV)

10 You, however, know all about my teaching, my way of life, my purpose, faith, patience, love, endurance, 11 persecutions, sufferings—what kinds of things happened to me in Antioch, Iconium and Lystra, the persecutions I endured. Yet the Lord rescued me from all of them. 12 In fact, everyone who wants to live a godly life in Christ Jesus will be persecuted, 13 while evildoers and impostors will go from bad to worse, deceiving and being deceived. 14 But as for you, continue in what you have learned and have become convinced of, because you know those from whom you learned it, 15 and how from infancy you have known the Holy Scriptures, which are able to make you wise for salvation through faith in Christ Jesus. 16 All Scripture is God-breathed and is useful for teaching, rebuking, correcting and training in righteousness, 17 so that the servant of God[a] may be thoroughly equipped for every good work.

In this life, Christians are facing hardships in order to live a life that matters for Christ. Therefore, we must arm ourselves with His attitude.

When a believer suffers because of his or her commitment to Christ, that believer has made a choice to be done with sin. That believer has made a choice to cease living a sinful lifestyle in order to live according to God’s will.


ALHAMISI TAREHE 8 JULAI 2021,     ASUBUHI                                 

2 TIMOTHEO 3:10-17

10 Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu,
11 na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
12 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.
13 lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
14 Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao;
15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

Katika maisha haya, Wakristo wanapitia magumu ili kuishi maisha yanayompendeza Kristo. Hivyo, ni lazima tujivike tabia ya Yesu Kristo. Mkristo anapoteswa kwa sababu ya kujitoa maisha yake kwa ajili ya Kristo, mtu huyu tayari amefanya uamuzi wa kuacha dhambi. Amechagua kuyaacha maisha ya uovu ili kuishi sawa na mapenzi ya Mungu.