JUMAMOSI TAREHE 19 JUNI 2021 ASUBUHI
Luka 17: 31-37
31 Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.
32 Mkumbukeni mkewe Lutu.
33 Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya.
34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
37 Wakajibu, wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai.
Katika somo la leo, Yesu alikuwa anajibu swali la wanafunzi wake kuhusu kuja kwa ufalme wa Mungu (Luka 17:20) Anapowajibu utaona kwamba hawatajua saa wala wakati ufalme wa Mungu utakapokuja. Yesu alitaka wanafunzi wake wasitumie nguvu zao kujua ufalme wa Mungu utakuja lini, bali wawe tayari wakati wote (Luka 17:31) Neno hili linatuhusu pia sisi wafuasi wa Kristo, tunapaswa kuwa tayari wakati wote, tukingojea ujio wa pili wa Kristo.
SATURDAY 19TH JUNE 2021, MORNING
Luke 17:31-37 New International Version
31 On that day no one who is on the housetop, with possessions inside, should go down to get them. Likewise, no one in the field should go back for anything. 32 Remember Lot’s wife! 33 Whoever tries to keep their life will lose it, and whoever loses their life will preserve it. 34 I tell you, on that night two people will be in one bed; one will be taken and the other left. 35 Two women will be grinding grain together; one will be taken and the other left.” [36] [a]
37 “Where, Lord?” they asked.
He replied, “Where there is a dead body, there the vultures will gather.”
Footnotes
- Luke 17:36 Some manuscripts include here words similar to Matt. 24:40.
In today's lesson, Jesus was answering his disciples' question about the coming of the kingdom of God (Luke 17:20). Jesus wanted His disciples not to use their strength to know when the kingdom of God would come, but to be ready at all times (Luke 17:31).
This also applies to us as followers of Christ, we must always be ready, waiting for the second coming of Christ.