Date: 
27-04-2021
Reading: 
Romans 10:8-13 (Warumi 10:8-13)

TUESDAY 27TH APRIL 2021    MORNING                                 

Romans 10:8-13 New International Version (NIV)

But what does it say? “The word is near you; it is in your mouth and in your heart,”[d] that is, the message concerning faith that we proclaim: If you declare with your mouth, “Jesus is Lord,” and believe in your heart that God raised him from the dead, you will be saved. 10 For it is with your heart that you believe and are justified, and it is with your mouth that you profess your faith and are saved. 11 As Scripture says, “Anyone who believes in him will never be put to shame.”[e] 12 For there is no difference between Jew and Gentile—the same Lord is Lord of all and richly blesses all who call on him, 13 for, “Everyone who calls on the name of the Lord will be saved.”[f]

Faith puts us right with God, but our verbal confession of the Lordship of Christ saves us. Confession is not a work we do which merits God’s favor. It is simply an act of obedience and evidence that one really does believe in Jesus Christ. Everyone who calls on the name of the Lord will be saved.


JUMANNE TAREHE 27 APRILI 2021     ASUBUHI                    

WARUMI 10:8-13

Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.
Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.
12 Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;
13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.

Imani inatupatanisha sisi na Mungu, lakini tunapokiri kwa midomo yetu kuwa Kristo ni Bwana, tunaokolewa. Kitendo cha kulikiri jina la Bwana siyo kazi inayosababisha tuhesabiwe haki na Mungu. Ukiri ni tendo la utii na uthibitisho kuwa tumemwamini Yesu Kristo. Kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.