Date: 
06-08-2021
Reading: 
Mithali 3:5-7

Ijumaa asubuhi 06.08.2021

Mithali 3:5-7

[5]Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, 

Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

[6]Katika njia zako zote mkiri yeye, 

Naye atayanyosha mapito yako.

[7]Usiwe mwenye hekima machoni pako; 

Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.

Mwenendo wenu uwe na hekima;

Leo asubuhi tunapewa maonyo juu ya kumwamini na kumheshimu Mungu. Ni wito kumtegemea Mungu na siyo akili zetu, naye atanyoosha njia zetu.

Somo linatufundisha kuwa sisi hatuna uwezo juu ya jambo lolote bila msaada wa Mungu. Kwa maana hiyo kumtegemea Mungu ni muhimu. Muhimu zaidi ni kuwa, katika huko kumtegemea Mungu, sharti tuache uovu. Siku njema.