Date: 
04-10-2022
Reading: 
Mithali 26:2

Jumanne asubuhi tarehe 04.10.2022

Mithali 22:6

[6]Mlee mtoto katika njia impasayo, 

Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Tuwajali watoto wetu;

Mtoto hujifunza kwa wazazi na(au) walezi wake. Hujifunza jinsi ya kuishi akitenda anavyoona kwa wakubwa. Njia mbaya humfundisha kutenda mabaya, kinyume chake pia. Ndiyo maana somo la asubuhi hii linaangazia kumlea mtoto katika njia impasayo ili adumu katika hiyo njia daima.

Unamleaje mtoto wako?

Tunawaleaje watoto wetu?

Maisha tunayoishi yanatakiwa kuwa kielelezo kwa watoto wetu, maana kwa njia hiyo wanajifunza. Tukiwalea katika njia ipasayo tunaandaa familia bora na Kanisa kwa ujumla, maana watakuwa ni watu wenye kumcha Bwana. Timiza wajibu wako, mlee mtoto wako katika njia sahihi.

Siku njema.