Date: 
08-09-2022
Reading: 
Mithali 21:23-24

Alhamisi asubuhi 08.09.2022

Mithali 21:23-24

[23]Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, 

Atajilinda nafsi yake na taabu.

[24]Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; 

Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.

Tutumie vizuri ndimi zetu;

Leo asubuhi tunasoma kuwa mtu azuiaye kutumia ulimi wake vibaya hujiepusha na taabu. Hii ni kwa sababu kutumia vibaya ulimi husababisha kumkosea Mungu, maana yake kutenda dhambi. Somo linaonesha kuwa mwenye kiburi na majivuno hutenda vibaya, ikiwemo kunena vibaya.

Tunapewa wito wa kutumia ndimi zetu vizuri ili tusiingie taabuni. Tupende kujifunza na kusikiliza maana tutapata maarifa yatakayotuongoza kuwaza vyema, hatimaye kutumia ulimi vizuri ili tuwe na mwisho mwema.

Siku njema.