Date: 
06-10-2022
Reading: 
Mithali 1:7-9

Alhamisi asubuhi tarehe 06.10.2022

Mithali 1:7-9

7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.

8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,

9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako.

Tuwajali watoto wetu;

Maisha yanayompendeza Bwana ni yale yenye kumcha yeye. Jamii inayomcha Bwana huwa na watu waadilifu, maana watu wote wakiwemo watoto hutenda mema. Jamii ya namna hii hushika mafundisho ya Bwana, hivyo watoto hukua katika maadili mema ya kumpendeza Bwana.

Hiyo ndiyo jamii tunayoitwa kuijenga leo. Jamii inayomcha Bwana na kushika mafundisho yake. Tunapowafundisha watoto kumcha BWANA, tunawapa urithi mzuri kwa maana kujenga jamii inayomcha Bwana. Timiza wajibu wako.

Siku njema.