Date:
07-10-2022
Reading:
Mithali 1:15-19
Ijumaa asubuhi tarehe 07.10.2022
Mithali 1:15-19
15 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
16 Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.
17 Kwa kuwa mtego hutegwa bure, Mbele ya macho ya ndege ye yote.
18 Na hao hujiotea damu yao wenyewe, Hujinyemelea nafsi zao wenyewe.
19 Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo.
Tuwajali watoto wetu;
Sura ya kwanza ya kitabu cha Mithali inaanza kwa kuonesha kuwa kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa. Mwanadamu anaitwa kujua hekima na adabu katika kumtumikia Bwana. Katika maarifa hayo, somo letu asubuhi hii linatuangazia kutoshirikiana na waovu.
Somo linatuita kujichunguza njia zetu (15) na kutowafuata waovu. Tuzuie miguu yetu isiende pamoja nao. Kuzuia huko ni kutoiga mabaya kwa wenzetu, na kutenda mazuri yanayomtangaza Kristo. Tusiwe wenye tamaa, bali wenye bidii katika kuutafuta uso wa Mungu na haki yake. Tuwe chachu ya haki.
Siku njema.