Date: 
10-07-2018
Reading: 
Matthew 5:25-26 (Mathayo 5:25-26)

TUESDAY 10TH JULY 2018 MORNING                                

Matthew 5:25-26 New International Version (NIV)

25 “Settle matters quickly with your adversary who is taking you to court. Do it while you are still together on the way, or your adversary may hand you over to the judge, and the judge may hand you over to the officer, and you may be thrown into prison. 26 Truly I tell you, you will not get out until you have paid the last penny.

We should try to resolve all disputes peacefully. Such disputes are often caused by selfishness. As Christians we should care about the views and interests of other people and not just push our own agenda.

May God help us to be peacemakers and to value harmony.

JUMANNE TAREHE 10 JULAI 2018 ASUBUHI                      

MATHAYO 5:25-26

25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. 
26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho. 
 

Mungu atusaidie kuishi kwa amani na watu wote. Kama tunakosana na ndugu au jirani tujishushe na tumsikilize. Tujali maoni na mahitaji ya watu wengine. Tusilazimishe mipango yetu kila wakati. Tukumbuke mara nyingi hali ya kutoelewana na ugomvi kati ya watu au makundi mawili inasababishwa na ubinafsi. Mungu atusaidie kujali na kuelewana.