Date: 
27-02-2019
Reading: 
Matthew 13:1-9 (Mathayo 13:1-9)

WEDNESDAY  27TH FEBRUARY 2019 MORNING                

Matthew 13:1-9 New International Version (NIV)

The Parable of the Sower

1 That same day Jesus went out of the house and sat by the lake.Such large crowds gathered around him that he got into a boat and sat in it, while all the people stood on the shore. Then he told them many things in parables, saying: “A farmer went out to sow his seed. As he was scattering the seed, some fell along the path, and the birds came and ate it up. Some fell on rocky places, where it did not have much soil. It sprang up quickly, because the soil was shallow. But when the sun came up, the plants were scorched, and they withered because they had no root. Other seed fell among thorns, which grew up and choked the plants. Still other seed fell on good soil, where it produced a crop—a hundred, sixty or thirty times what was sown. Whoever has ears, let them hear.”  

18 “Listen then to what the parable of the sower means: 19 When anyone hears the message about the kingdom and does not understand it, the evil one comes and snatches away what was sown in their heart. This is the seed sown along the path. 20 The seed falling on rocky ground refers to someone who hears the word and at once receives it with joy. 21 But since they have no root, they last only a short time. When trouble or persecution comes because of the word, they quickly fall away. 22 The seed falling among the thorns refers to someone who hears the word, but the worries of this life and the deceitfulness of wealth choke the word, making it unfruitful. 23 But the seed falling on good soil refers to someone who hears the word and understands it. This is the one who produces a crop, yielding a hundred, sixty or thirty times what was sown.”

Jesus often taught in parables but He did not always explain the meaning of the parables. He wanted people to think deeply about what He was saying. Here Jesus gives us both the parable and its meaning.

Think about this. How much Good seed has been sown in your life? Which kind of soil are you?

JUMATANO TAREHE 27  FEBRUARI 2019 ASUBUHI   

MATHAYO 13:1-9, 18-23

1 Siku ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari. 
Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani. 
Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. 
Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; 
nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; 
na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka. 
Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; 
nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. 
Mwenye masikio na asikie. 

18 Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi. 
19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia. 
20 Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; 
21 lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa. 
22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai. 
23 Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini. 

Yesu mara kwa mara alifundisha kwa mifano. Mara nyingi hakutoa maana ya mifano yake. Alitaka wasikiliziaji kutafakri sana kuhusu maana yake. Katika somo hapo juu tunasoma mfano na maana yake.

Jichunguze. Mara ngapia mbegu bora imepandwa katika maisha yako? Je! Wewe ni udongo aina gani?