Date: 
27-07-2022
Reading: 
Mathayo 7:1-5

Jumatano asubuhi tarehe 27.07.2022

Mathayo 7:1-5

[1]Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.

[2]Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.

[3]Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?

[4]Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?

[5]Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Amri mpya nawapa, Mpendane 

Yesu alijua maisha ya waliomfuata, kuwa walihukumiana wao kwa wao. Waliishi maisha ya mmoja kuona makosa ya mwenzake bila kuona ya kwake. Ndiyo maana tunasoma asubuhi hii akiwaambia kuwa mtu ajitoe boriti kwanza kwenye jicho lake, ndipo ajiangalie mwenyewe.

Yesu hakumaanisha tusisaidiane.

Yesu hakumaanisha kila mtu akae peke yake.

Yesu hakusema tusijuane.

Yesu alimaanisha kuwa kila mtu ajitunze katika yeye (Yesu Kristo) ikiishi inavyompendeza Mungu. Kwamba kila mtu akijitunza mwenyewe, tutakuwa na Kanisa la watu wanaomcha Mungu, wanaopendana, wasiohukumiana bali kuonyana na kuelekezana kwa upendo. Linda sana moyo wako, mpende jirani yako.

Jumatano njema