Date: 
18-01-2023
Reading: 
Mathayo 5:8-13

Jumatano asubuhi tarehe 18.01.2023

Mathayo 8:5-13

[5]Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,

[6]akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.

[7]Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.

[8]Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

[9]Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

[10]Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.

[11]Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;

[12]bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

[13]Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile.

Nyumba zetu hubarikiwa na Mungu;

Akida alikuwa na mtumishi ambaye alikuwa mgonjwa nyumbani kwake. Huenda alikuwa amekwisha mpeleka sehemu tofauti kupata tiba pasipo mafanikio. Lakini baada ya kusikia habari za Yesu, alimfuata kwa Imani akimuomba amponye mtumishi wake. Mstari wa 8 unaonesha Imani ya akida yule;

Mathayo 8:8

[8]Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

Yesu alishuhudia akisema Imani ya yule akida ilikuwa kubwa sana!

Tunaloliona hapa ni kuwa yule akida aliamua kumpelekea Yesu shida ya nyumbani kwake, yaani mgonjwa wake, na Yesu kama kawaida yake alimponya. 

Tunafundishwa kumpelekea Yesu shida zetu tulizonazo nyumbani kwetu, maana yeye ndiye msaada. Haimaanishi tusiwajibike, bali tutimize wajibu wetu, tukimtegemea Mungu katika yote.

Jumatano njema 

 

Heri Buberwa 

Mlutheri