Date: 
22-11-2021
Reading: 
Mathayo 25:14-25 (Matthew)

JUMATATU TAREHE 22 NOVEMBA 2021, ASUBUHI

Mathayo 25:14-25

14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.
15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
16 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.
17 Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.
18 Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake.
19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.
20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida.
21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.
23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.

Uzima wa Ulimwengu ujao;

Yesu alitoa mfano wa talanta, ambapo watumwa wawili walikuwa waaminifu katika mali waliyopewa na bwana wao, wakazalisha, na bwana wao akawaweka juu ya mengi.

Mmoja alifukia talanta yake, hakuifanyia kazi. Bwana wake  hakupendezwa na mtumwa wake huyo aliyefukia talanta, akaamuru anyang'anywe hiyo talanta moja apewe yule aliyezalisha tano zikawa kumi.

Tunaitwa kutumia vipawa tulivyopewa kwa ajili ya Bwana, kama wale wawili waliozalisha talanta zao zaidi, maana kazi yake inatuhusu. Yule aliyefukia talanta ni alama ya watu wavivu wasiofanya kazi, lakini wenye imani haba, maana hakuwa na imani wala utii kwa bwana wake.

Tafsiri pana ni kuwa watendakazi waaminifu wa Mungu, ili siku akirudi tuwe tayari kwa ajili ya uzima wa Ulimwengu ujao.

Uwe na wiki njema yenye ushuhuda.


MONDAY 22ND NOVEMBER 2021, MORNING

Matthew 25:14-25

The Life of the World to Come;

Jesus gave the parable of the talents, in which two slaves were faithful in a master's household, producing profit with the money entrusted, and the master entrusted them with much more.

One hid the money he was given, he did not make profit. His master did not want his slave to cover his money, so he ordered that of the money be given to him who had produced more.

We are called to use the talents  we have been given for the Lord, like the two who produced most profit, for his work concerns us. The one who hides his talent is a symbol of lazy people who do not work, who have little faith, because he has no faith or obedience to his master.

The broad definition is to be faithful servants of God, so that when He returns we may be ready for the life of the world to come.

Have a good week with testimonials.