Date: 
05-12-2022
Reading: 
Mathayo 25:1-13

Hii ni Advent;

Jumatatu asubuhi tarehe 05.12.2022

Mathayo 25:1-13

1 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.

2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.

3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;

4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.

5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.

6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.

7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.

8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.

9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.

10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.

12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.

13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.

Bwana anakuja katika Utukufu wake;

Asubuhi ya leo tunaanza juma kwa mfano wa wanawali kumi waliomngoja Bwana harusi, watano wakiwa na mafuta kwenye taa zao, watano wakiwa hawana. Ilipofika usiku wa manane ilibidi wale wasio na mafuta wakanunue, na waliporudi hawakuweza kuingia kwenye sherehe maana mlango ulikuwa umefungwa tayari. 

Wale watano waliokuwa na mafuta kwenye taa zao ni picha ya watu wanaojiandaa kumpokea Kristo. Wameandaa mioyo yao, wakimcha Bwana kwa kutenda mema. Ambao hawakuwa na mafuta ni picha ya wale ambao hawajiandai kumpokea Bwana atakaporudi. Hawasomi neno la Mungu, wengine hawaendi ibadani kumwabudu Mungu na kujifunza, hawatendi yawapasayo wakristo, yaani mioyo yao haiko tayari kumpokea Bwana. Wewe uko kundi lipi? 

Tembea na swali hili leo;

"Taa yako ina mafuta?"

 

Uwe na wiki njema.