Date: 
12-10-2022
Reading: 
Mathayo 12:1-8

Jumatano asubuhi tarehe 12.10.2022

Mathayo 12:1-8

1 Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala.

2 Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.

3 Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe?

4 jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?

5 Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia?

6 Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.

7 Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia.

8 Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.

Kristo ametuweka huru;

Wanafunzi walivunja masuke mashambani wakala siku ya Sabato, jambo ambalo Mafarisayo hawakuliunga mkono. Walimweleza Yesu juu ya uvunjifu huu wa Torati. Yesu ndipo akawapa mfano wa Daudi alivyotenda isivyostahili hekaluni, lakini hakuwa na hatia! 

Mafarisayo waliifuata torati, lakini Yesu ndiye aliyekuwa mtimilifu wa torati kama alivyosema;

Mathayo 5:17;  Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.

Kwa maana hiyo walitakiwa kumwamini na kumfuata Yesu. Badala yake walikuwa watu wa kuhoji kila kitu.

Sisi hatuko chini ya sheria, bali tumeokolewa na Yesu Kristo kwa njia ya kifo msalabani. Kumbe wajibu wetu ni kumwamini na kumfuata. Sisi tusihoji kama Mafarisayo, bali tuutafute uso wake kwa maisha yetu ya sasa na baadaye, maana tayari Kristo ametuweka huru toka dhambini.

Siku njema