Date: 
29-12-2021
Reading: 
Matendo 6:7-15

Jumatano asubuhi 29.12.2021

Matendo ya Mitume 6:7-15

7 Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.

8 Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.

9 Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;

10 lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye.

11 Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu.

12 Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.

13 Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati;

14 maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu mahali hapa, na kuzibadili desturi tulizopewa na Musa.

15 Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika.

Stefano shahidi mwaminifu wa Yesu;

Stefano shahidi mwema na mwaminifu alijaa neema, akitenda maajabu na ishara kwa jina la Yesu. Alimtangaza Yesu lakini alikataliwa! Hadi kupigwa mawe! 

Stefano hakukata tamaa hudumani, pamoja na vikwazo vyote hivyo. Alisimamia kweli ya Mungu bila woga. Aliwahubiria akitoa historia, toka Yesu alivyozaliwa hadi wakamsulibisha, wakachomwa mioyo yao na kuchukia, wakampiga mawe hadi kufa.

Tunaitwa kuwa mashahidi waaminifu wa Yesu;

1. Kwa kuwasikiliza watenda kazi wa Mungu. Hapo ndipo tunapata maarifa ya jinsi ya kuishi na kumpendeza Mungu. Kuishi kwa kumpendeza Mungu ndio ushuhuda mwema kwa Yesu Kristo.

2. Kwa kutoiacha njia sahihi katika kumfuata Kristo. Stefano anatufundisha kutokata tamaa katika utume huu tulioitiwa. Vikwazo ni vingi, lakini tuombe kujazwa neema na uwezo utokao kwa Mungu ili tuweze kuwa mashahidi waaminifu wa Yesu.

Nakutakia Jumatano njema.