Date: 
19-01-2022
Reading: 
Matendo 10:17-23

Jumatano asubuhi tarehe 19.01.2022

Matendo ya Mitume 10:17-23

17 Hata Petro alipokuwa akiona shaka ndani ya nafsi yake, maana yake ni nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiisha kuiulizia nyumba ya Simoni, wakasimama mbele ya mlango,

18 wakaita; wakauliza kwamba Simoni aitwaye Petro anakaa humo.

19 Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta.

20 Basi ondoka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma.

21 Petro akawashukia wale watu, akanena, Mimi ndiye mnayemtafuta. Mmekuja kwa sababu gani?

22 Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mchaji wa Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno kwako.

23 Akawakaribisha wawe wageni wake. Hata siku ya pili, Petro akaondoka akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yafa wakafuatana naye.

Mungu hutakasa nyumba zetu;

Kronelio alituma watu kumfuata Petro aende nyumbani kwake. Petro alikubali wito akiongozwa na Roho wa Mungu (19-20). Kwa kumtii Mungu, akafuata maelekeze ya Roho Mtakatifu kwa kuondoka na ujumbe wa Kronelio kuelekea Kaisaria.

Petro alifanya uamuzi wa kwenda kwa Kronelio kwa kuelekezwa na Roho Mtakatifu. Inaonesha hapa Petro alimtegemea Mungu katika utume wake. Kumbe nasi tukimsikiliza na kumtegemea Mungu anabariki nyumba zetu.

Jumatano njema.