MATANGAZO YA USHARIKA
LEO TAREHE 07 AGOSTI, 202
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
MLANGO WA KUINGIA MBINGUNI
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.
3. Matoleo ya Tarehe 31/07/2022
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yak
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO
0757 391174 - KKKT AZANIA FRON
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRA
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.
5. Uongozi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, unapenda kuwataarifu kwamba, kutakuwa na Semina ya Wawakilishi wa Mfuko wa Elimu pamoja na Viongozi wa Jumuiya Sharika na Mitaa itakayofanyika kwa Majimbo yote sita(6) ya DMP. Jimbo la kati itakuwa tarehe 27/08/2022 saa tatu asubuhi Usharika wa Kariakoo. Viongozi wote wa Jumuiya mnaombwa kuhudhuria bila kukosa semina hii muhimu.
6. Leo tarehe 07/08/2022 tutamtolea Mungu fungu la Kumi. Washarika karibuni.
7. Jumapili ijayo tarehe 14/08/2022 ni siku ya ubatizo wa watoto wadogo na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.
8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
Kwa mara ya pili tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 20/08/2022
SAA 09:00 ALASIRI
Bw. John Ezekiel Mfugale na Bi. Tumaini Heric
Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.
9. NYUMBA KWA NYUMBA
- Masaki na Oyserbay: Kwa Bwana na Bibi Seppi MawallMakumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Ruth Korosso.
- Mjini kati: watafanya kwa njia ya Mtandao.
- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Mony.
- Kinondoni: Watatangaziana.
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mujuni Mutembei.
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi George Kinyaha
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Dr. na Bibi Kumbwaeli Salewi.
10. Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili.
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.