MATANGAZO YA USHARIKA

                                                     TAREHE 06 FEBRUARI, 2022

                                           NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

                                                  UTUKUFU WA MWANA WA MUNGU 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Tumepokea wageni 3 waliotufikia na vyeti.

3. Matoleo ya Tarehe 30/01/2022

    Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali                alizotupa kwa kazi yake.

    NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

    0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

    Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu pamoja na Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.30 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Kwaya ya Agape itatembelea watoto wenye uhitaji maalum (Vichwa vikubwa na mgongo wazi) tarehe 22/02/2022 kwa kuwasaidia kupata Bima za Afya Watoto sabini (70) ambao kila mmoja ni Tshs. 50,400/=. Pia na vitu mbalimbali kama sabuni za kuogea, sabuni za kufulia, mafuta ya kupaka, nguo safi n.k Kwaya inaomba washarika muwaunge mkono. Vitu vyote vipelekwe kwa Mhasibu au ofisi ya Parish Worker. Mungu awabariki.

6. Leo tarehe 06/02/2022 Tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

7. Jumapili ijayo tarehe 13/02/2022 ni siku ya ubatizo wa watoto wadogo na kurudi kundini. Watakao hitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

8. Kamati ya Uhusiano na Habari inapenda kuwashukuru wote ambao wametoa michango yao ya kuboresha Chanel yetu ya Azania Front TV. Aidha inawakumbusha wale ambao hawajarejesha kadi za michango walizochukua warejeshe mapema. Pia wanaohitaji kadi hizo bado zipo Wazee wa kanisa wanazo watazigawa kwa wale wanaohitaji. Mungu awabariki kwa ushirikiano mzuri.

9. Idara ya Sanaa na michezo hapa Usharikani inapenda kuwatangazia vijana wote kuwa watakutana siku ya jumatatu tarehe 07/02/2022 yaani kesho saa 11.00 jioni kwa ajili ya maandalizi ya Igizo la Pasaka. Mazoezi yatakuwa ni kila siku ya jumatatu na jumamosi. Vijana wote mnakaribishwa na Mungu awawezeshe.

10. Shukrani

Jumapili ijayo tarehe 12/02/2022 katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi familia ya Mzee Raymond Sangiwa watamshukuru Mungu baada ya mke wake Mama Elizabeth Sangiwa kuponywa ugonjwa wa ganzi mwilini uliomsumbua kwa muda mrefu, kuwavusha salama Mwaka 2021, kumaliza salama msiba wa mjukuu wao uliotokea mwezi Januari 2022 na mengine mengi aliyowatendea.

Neno: Zaburi 103:1-3, Wimbo: TMW 29

11. NYUMBA KWA NYUMBA

Masaki na Oyserbay: itafanyika jumatano ijayo tarehe 09/02/2022 kwa Judge na Bibi Juxon Mlay .

12. NDOA.

Matangazo ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

13. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Pili.

                        Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.