MATANGAZO YA USHARIKA
LEO TAREHE 28 NOVEMBA, 2021
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
BWANA ANALIJIA KANISA LAKE.
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.
3. Matoleo ya Tarehe 21/11/2021
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu pamoja na Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.30 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu
6. Leo tutashiriki chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.
7. Jumapili ijayo tarehe 05/12/2021 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Aidha siku hiyo ibada itakuwa ni moja itakayoanza saa 1.00 asubuhi, ikiambatana Mkutano Mkuu wa Usharika. Washarika tuiombee siku hiyo.
8. Uongozi wa Umoja wa Vijana unapenda kuwatangazia Vijana wote kuwa kutakuwa na semina tarehe 09/12/2021 kuanzia saa 2 asubuhi. Hivyo wanaomba vijana waliotayari wajiandikishe majina yao kwa uongozi wa Umoja wa Vijana kwa ajili ya Maandalizi. Sehemu itakapofanyika semina vijana watajulishwa.
9. Wazazi na Walezi wenye watoto wanaoanza Kipaimara mwaka wa Kwanza 2022 wafike Ofisi ya Parish Worker ili wajiandikishe. Umri ni kuanzia miaka 12 na kuendelea.
10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini Kati: Kwa njia ya Mtandao
Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Mama Mamkwe.
11. NDOA.
NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 18/12/2021
SAA 8.00 MCHANA
Bw. Emmanuel Melckizedeck Sanare na Bi. Agatha Silas Kaaya
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 04/12/2021
SAA 10.00 JIONI
Bw. Emmanuel Benson Jonas na Bi. Florida Renatus Kyando
NDOA IFUATAYO ITAFUNGWA USHARIKA WA GEZAULOLE DAYOSISI YA KASKAZINI KATI YA
Bw. Anold Weransari Kimambo na Bi. Aikande Elisante Lema
VILE VILE NDOA IFUATAYO ITAFUNGWA CCT CHAPLAINCY CHUO KIKUU UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Bw. Mulashani Emanzi Bikombo na Bi. Anna Emmanuel Mbijima
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
11. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Kwanza
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.