MATANGAZO YA USHARIKA
LEO TAREHE 27 MACHI, 2022
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
YESU NI MKATE WA UZIMA
1.Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2.Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.
3. Matoleo ya Tarehe 20/03/2022
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu, pamoja na Semina zinazoendelea kipindi chote cha Kwaresma siku ya Alhamisi na Ijumaa pamoja na Maombi na Maombezi saa 11.30 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.
5. Leo tarehe 27/03/2022 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.
6. Uongozi wa umoja wa wanawake , unawaomba wanawake wote walio katika vikundi vya uimbaji na wasio katika vikundi, wajiunge katika kwaya ya wanawake usharikani kwa ajili maandalizi ya uimbaji wa tamasha la pasaka. Siku za mazoezi ni jumatano na ijumaa kuanzia saa kumi kamili jioni. Aidha T-shirt za Ijumaa Kuu zipo kwa size zote. Bei ni sh elf 15 kwa wakubwa na elf 10 kwa watoto. Karibuni.
7. Shukrani:
Jumapili ijayo tarehe 03/04/2022 familia ya Mama Miriam Luhui watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyomtendea.
Neno: Zab.23, Wimbo: Yesu ni rafiki wa kweli (Kwaya ya Upendo)
8. Jumamosi ijayo tarehe 02/04/2022 saa 3.00 asubuhi kutakuwa na ibada Maalum ya Wazee itakayoambatana na Meza ya Bwana. Umri ni kuanzia Miaka 65. Wazee watakaohitaji usafiri waandike majina kwa Mzee wa Usharika au ofisini kwa Parish Worker.
9. NYUMBA KWA NYUMBA
- Masaki na Oyserbay: Watashiriki ibada ya jumatano hapa Usharikani
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa
- Mjini kati: watafanya njia ya Mtandao.
- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Watashiriki semina hapa Usharikani
- Kinondoni: Kwa Mama Hilda Rwezaula
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mcharo Mlaki
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Tom NJau
9. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Kwanza.
Pamoja na kuhudumu ibada ya Jumatano
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.