MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 21 AGOSTI, 2022
NENO LINALOTUONGOZA JUMA HILI NI
TUTUMIE VIZURI NAFASI TULIYOPEWA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.
3. Matoleo ya Tarehe 14/08/2022
4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
5. NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
6. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.
7. Jumapili ijayo tarehe 28/08/2022 tutashiriki chakula cha Bwana. Washarika tujiandae. Aidha siku hiyo itakuwa siku ya Uchaguzi wa Baraza la wazee. Washarika tuiombee siku hiyo.
8. Uongozi wa Kwaya ya Uinjilisti Agape unapenda kuleta ombi kwa Waimbaji na Washarika kuungana nao kwa ajili ya mazoezi ya maandalizi ya uimbaji wa kwaya za Uinjilisti ngazi ya Dayosisi. Siku za Mazoezi ni Jumatano saa 11.00 jioni, Jumamosi saa 6.00 Mchana na Jumapili mara baada ya ibada ya Kwanza. Wote mnakaribishwa.
9. SHUKRANI: JUMAPILI IJAYO TAREHE 28/08/2022
IBADA YA KWANZA
Viongozi wa umoja wa vijana waliomaliza muda wao watatoa shukrani ya pekee kumshukuru Mungu kwa kuweza kuwaongoza kipIndi chote cha uongozi wao wa miaka 4.
Wimbo: Kwaya ya Vijana
IBADA ZOTE TATU
Washiriki wa Huduma ya International Bible Study Fellowship (BSF) ambao baadhi yao ni Washarika wa Ibada zetu tatu, wameguswa kuja mbele za Bwana kwa sifa na Shukrani kwa kuuona uwepo wa Mungu katika mwaka wao wa Mafunzo (2021-22), na sasa wanakaribia kuanza mwaka mpya 2022-23, Kipekee, wanamshuhudia Mungu kwa kuwatuma kupeleka upendo wake kwa wenye shida, walio gerezani.
Wimbo: Wataimba wenyewe
IBADA YA TATU.
Familia ya Dada Edith Mashasi Michael watamshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kuwatia nguvu tangu mume wake mpendwa alipotwaliwa na Bwana miaka kumi iliyopita, watoto kufanya vizuri katika mitihani yao na uponyaji wa wazazi waliokuwa India kwenye matibabu.
Wimbo: Nitayainua Macho yangu( Kwaya Kuu)
Familia ya Christina Paul Kiboma watamshukuru Mungu kwa kuendelea kumtunza Baba yao Mzee Kiboma na kutimiza miaka 82, kumlinda mtoto Angel Maria Peter, Chrisha Imani kufikisha miaka 4 tarehe 28/08. Pamoja na mambo mengine mengi aliyowatendea.
Neno: Zaburi 64:1-2, Wimbo: TMW 196
10. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
Kwa mara ya Kwanza tunatangaza Ndoa ya tarehe 10/09/2022
SAA 9.00 ALASIRI
Bw. Peter Tom Njau na Bi. Jacqueline Abiudi Nkya
Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.
11. NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evattt Kuzilwa.
- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa ………………………
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Tom Njau
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Elisha Mushumbusi
12. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.