MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 20 FEBRUARI, 2022
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
NENO LA MUNGU LINA NGUVU NI UPANGA UKATAO KUWILI
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.
3. Matoleo ya Tarehe 13/02/2022
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu pamoja na Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.30 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.
5. Jumapili ijayo tarehe 27/02/2022 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae
6. Shukrani -
Jumapili ijayo tarehe 27/02/2022
Ibada ya tatu saa 4.300 asubuhi
Familia ya marehemu David Goodwill Korosso na Bibi Masala Korosso watamshukuru Mungu kwa faraja, amani ya moyo anayozidi kuwapa familia, ndugu, jamaa na marafiki, kuendelea kuwasimamia tangu mpendwa wao David Goodwill Korosso alipotwaliwa na Bwana Mwaka mmoja uliopita 10/02/2021 pamoja na mambo mengi anayoitendea familia yake na anayozidi kuwatendea.
Neno: 1Wathesalonike 5:18, TMW 424 (Nionapo amani kama shwari)
7. NYUMBA KWA NYUMBA
Masaki na Oyserbay: itafanyika kwa Mama Nsile Mollel.
Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa ……………………………………….
Mjini kati watafanya kwa njia ya Mtandao.
8. NDOA.
Matangazo ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
9. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Pili.
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.