MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 19 JUNI, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

MSIGOMBANE NJIANI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.

3. Matoleo ya Tarehe 12/06/2022

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

6. Uongozi wa shule ya Jumapili unapenda kuwashukuru sana Wazazi kwa kuwaandaa watoto kwa ajili ya Tamasha lililofanyika jana Jumamosi Tarehe 18/06/2022. Mungu awabariki.  

7. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

Hakuna Ndoa za washarika

8. Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.

SHUKRANI: 

Jumapili ijayo tarehe 26/06/2022 katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi familia ya Bwana na Bibi Mapunda watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na Uponyaji.

Neno: Zaburi 25:1-5, Wimbo: TMW 298 (Kwa huruma nikubali)

9. NYUMBA KWA NYUMBA

- Masaki na Oyserbay: Kwa Bwana Witson Moshi

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Matee

- Mjini kati: watafanya njia ya Mtandao.

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi George Msuya

- Upanga: Kwa Mama Violet Maro

10. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki