MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 15 JANUARI, 2023
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
NYUMBA ZETU HUBARIKIWA NA MUNGU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 08/01/2023
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wakumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.
5. Kwaya ya Agape/walezi wa kwaya watatembelea wahitaji katika hospital ya muhumbili ,wakilenga zaidi kuwafikia watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wapatao 100 kwa kuwachangia bima ya afya kwa kila mtoto gharama yake ni sh @50,400/= pamoja na vitu kama sabuni, mafuta ya kupata,miswaki,nguo size mbali mbali,juice,maji nk, Wanaomba washarika muwaunge mkono kwenye huduma hii, Ofisi ya Parish weka na mhasibu itapokea sadaka hii Mungu awabariki.
6. SHUKRANI - JUMAPILI TAREHE 22/01/2023
KATIKA IBADA ZOTE
Umoja wa Wanawake watamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kumaliza Mwaka 2022 na kuingia Mwaka 2023.
Neno: Isaya 12, Zaburi 138:1-3, Wimbo: 295
7. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Oysterbay na Masaki: Kwa Mzee Malentlema
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:
- Kwa Mzee Evatt Kuzilwa
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Adv. Joseph na
Mzee Vupe Mpuya
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Tom Njau
8. NDOA.
Hakuna Ndoa za Washarika
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.
9. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.