MATANGAZO YA USHARIKA

  TAREHE 10 JUNI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI 'WITO WA KUINGIA UFALME WA MUNGU'

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti.

3. Alhamisi ijayo tarehe 14/06/2018 kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi yatakayoanza saa 11.30 jioni. Wote mnakaribishwa.

4. Vitenge vya umoja wa Wanawake  vya Dayosisi vipo ambavyo  vitatumika kwa matukio yote ya Wanawake. Bei ni shilingi 25,000/= tu. Vitapatikana hapo nje.

5. NDOA.

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 30/06/2018

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. John Ndisha Furahini               na     Bi Anneth Adolph Makenja

 

NDOA HII IFUATAYO ITAFUNGWA KANISA LA KATOLIKI PAROKIA YA UPANGA.

Bw. Derick Mujuni Kajukano           na     Bi. Anita Abednego Kinasha

 

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

6. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Abraham Salewi
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Elinafika Mkumbwa
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Kowero
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Felix Mosha
  • Mjini kati:  Kwa Mama  Hilda Rwanshane
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Simon Jengo

                                              

7. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.