MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 10 APRIL, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

HOSANA NDIYE MBARIKIWA, AJAYE KWA JINA LA BWANA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti. 

3. Matoleo ya Tarehe 03/04/2022

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

6. NYUMBA KWA NYUMBA

- Masaki na Oyserbay: Watashiriki ibada ya jumatano hapa Usharikani

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Watatangaziana

- Mjini kati: watafanya njia ya Mtandao.

- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Watatangaziana

-Kinondoni: Kwa Profesa na Bibi S. Kulaba

- Upanga: Watashiriki ibada Kanisani siku ya Ijumaa.

7. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZITAKAZOFUNGWA TAREHE 30/04/2022  

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Heri Willy Mwakisole na Bi. Rehema Ismaily Mohamed

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo.

8. Familia ya Bwana na Bibi Makere wamepata zawadi ya watoto mapacha wa kike Ijumaa iliyopita. Wazazi na Watoto wanaendelea vizuri.

9. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.