MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 25 MARCH, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI WOTE SHANGILIENI BWANA ANAKUJA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Uongozi wa Kanisa Kuu Azania Front unapenda kumshukuru Mungu kwa kutupa wiki sita za kuketi miguuni pake kujifunza  juu ya Nguvu na Uweza wa damu ya Yesu, na maarifa juu ya kuitumia.  Masomo hayo yalifanyika kupitia semina zilizofanyika kila Jumatano, Alhamisi na Ijumaa ya kila wiki katika muhula huu wa kwaresma.  Tunawapongeza wote waliojaliwa kuhudhuria semina hizi na tunaamini kuwa imani juu ya nguvu na uweza wa Damu ya Yesu, na maarija juu ya kuitumia vimejengeka kwa upya.  Aidha tunamshukuru Mungu kwa kuwatumia watumishi wake kuwasilisha neno lake kwetu.  Kwa kulitambua hilo, siku ya Alhamisi tarehe 29.03.2018; kuanzia saa 11.00 hadi saa 12.30 jioni hapa Usharikani tutakuwa na maombi ya

- Kumshukuru Mungu kwa kutupa semina hii na afya na nguvu za kuhudhuria.

- Kuadhimisha Karamu ya Mwili na Damu ya Yesu, ambayo ibada yake itafanyika baadaye saa 1.00 jioni.

- Kumsihi Mungu kupitia semina hii ifanyike kitu kipya katika kudhihirisha uaminifu wake hapa Kanisa Kuu Azania Front   kupitia semina hii. 

- Washarika wote mnaalikwa kuhudhuria.

4. Uongozi wa Usharika  unapenda kuwashukuru washarika wote wenye umri kuanzia miaka 65 na kuendelea waliohudhuria ibada   maalum iliyofanyika jana tarehe 24/03/2018 saa 4.00 asubuhi.  Mungu awabariki sana.

5. Jumatano ijayo tarehe 28/03/2018 tutaendelea na ibada ya kwaresma.  Jumuiya ya TABATA NA WAZO/TEGETA/KUNDUCHI/BAHARI BEACH/UNUNIO itaongoza Liturgia. 

6. Jumatatu ya Pasaka tarehe 02/04/2018 kutakuwa na ibada ya  ni siku ya Tembea na yesu mfufuka itakayofanyika Mabibo External kuanzia saa 7.00 mchana. Wanawake wote wa Dayosisi watahudhuria hivyo wanawake wote hapa Usharikani tuungane na wenzetu kufanikisha ibada hii.   Ibada itaongozwa na Baba Askofu Dr. Alex G. Malasusa.

7. Mazoezi ya maandalizi ya Kantate yameshaanza kila siku ya Jumanne kuanzia saa 11.00 jioni. Wanakwaya wa Kwaya zote za mnaombwa kuhudhuria.

8. Tarehe 07/04/2018 saa 3.00 asubuhi kutakuwa na Kikao cha VICOBA ya Wajane na Wagane. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria kikao hiki muhimu.

9. Jumapili ijayo tarehe 01/04/2018 ni sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo. Ibada zitakuwa ni mbili kama kawaida saa 1.00 asubuhi na 3.30 asubuhi. Aidha siku hiyo tutamtolea Mungu fungu la Kumi.  Washarika tujiandae.

10. NDOA.

Hakuna ndoa za washarika.  Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi T. Onesmo

- Mjini kati:  Kwa  Mama Kabezi

- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa  Bwana na Bibi Masala Korosso

                                              

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.  

 

RATIBA YA PASAKA 2018

 

 

SIKU

 

 

  1.  

 

MUDA

 

MHUSIKA

ALHAMISI

29 MACHI, 2018

 

IBADA YA KUWEKWA

CHAKULA CHA BWANA

 

 

SAA 1.00 USIKU

 

 

IJUMAA KUU

30 MACHI, 2018

IBADA KAWAIDA

 

SAA 2.00 ASUBUHI

 

 

IGIZO,MISTARI YA MOYO

SAA 8.00 MCHANA

 

 

 

JUMAPILI

01 APRILI, 2018

 

IBADA KAMA KAWAIDA YA KWANZA

 

IBADA YA PILI

 

 

SAA 1.00 ASUBUHI

 

SAA 3.30 ASUBUHI

 

 

JUMATATU

02 APRILI, 2018

 

IBADA  MOJA ITAAMBATANA NA

UBATIZO

 

SAA 2.00 ASUBUHI

 

 

 

 

TEMBEA NA YESU MFUFUKA

 

SAA 8.00 MCHANA