KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA

DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 08 MEI, 2016

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI KUNGOJEA AHADI YA ROHO MTAKATIFU

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia na Cheti :
 1. Uongozi  wa shule ya jumapili unapenda kuwakumbusha wazazi kuwa jumamosi ijayo tarehe 14/05/2016 ndio siku ya tamasha la watoto Kijimbo litakalofanyika Usharika wa Ukonga.  Hivyo tunaomba watoto wote wanaoimba waletwe hapa kanisani saa 12.30 asubuhi.
 1. Jumapili ijayo tarehe 15/05/2016 katika ibada ya pili familia ya Dr. Benjamin L. Mtinangi watatoa shukrani ya pekee kwa mambo makuu Mungu aliyowatendea. Neno: Zaburi 118:28-29
 1. NDOA:

KWA MARA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 28.05.2016

      Bw. Francis Watson Mwaitembo  na     Bi. Happy Yonah Mwalusamba

NDOA HII ITAFUNGWA K.K.K.T USHARIKA WA MOSHI MJINI KANISA KUU

Matangazo mengine yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga:  Kwa bwana na Bibi Tom Njau
 • Kinondoni: Watatangaziana
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni Watatangaziana
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Mchungaji Mzinga
 • Oysterbay/Masaki: kwa Mama Chipeta
 • Tabata: Watatangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Watatangaziana Mjini kati: Hapa Usharikani
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: kwa Bwana na Bibi P. Mlagha