MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 08 JANUARI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI: WABATIZWAO NDIO WANA WA MUNGU.

 

  1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
  1. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti:
  2. Ibada ya Maombi na maombezi leo haitakuwepo mpaka tarehe 26/01/2017.
  1. Wazazi na Walezi wenye watoto wanaoanza Kipaimara mwaka wa Kwanza 2017 wafike ofisi ya Parish Worker ili wajiandikishe.
  1. Jumamosi ijayo tarehe 14/01/2017 kutakuwa na ibada ya pamoja ya nyumba kwa nyumba (jumuiya) zote kwa kuanza mwaka mpya wa 2017. Ibada hii itaanza saa 2.00 asubuhi.  Wote mnaombwa kuhudhulia ibada hii muhimu.
  1. Jumapili ijayo tarehe 15/01/2017 katika ibada ya pili, walimu wa shule ya jumapili watamshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyowatendea na kuwavusha mwaka 2016 salama na kuingia mwaka 2017.

Neno: Zab. 134:1-3,

Pia familia ya Dr. Lema nao watamshukuru Mungu tarehe 15/01/2017 katika ibada ya pili kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na Uponyaji wa Mama Rachel Lema.

Neno: Zab. 121:1-8, Wimbo: 295

  1. NDOA:

Matangazo ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu