KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA

DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

 TAREHE 06 NOVEMBA, 2016

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI UENYEJI WA MBINGUNI

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni: Wageni waliotufikia na Cheti ni
  1. Debora Ngilwangwa – toka usharika wa Ilembula Dayosisi ya Kusini. Amekuja kikazi.
  2. Oneska James Mbwile – toka Usharika wa Kanisa Kuu Tukuyu Mbeya Dayosisi ya Konde. Amekuja masomoni.

Kama kuna wageni wengine walioshiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.

 1. Leo tutamtolea Mungu fungu la kumi.
 1. Jumapili ijayo tarehe 13/10/2016 kutakuwa na ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji. Aidha siku hiyo familia ya Bi Mary Kinisa itamshukuru Mungu kwa mambo mengi makuu aliyowatendea ikiwa ni paoja na kupata mtoto, kutoka salama katika oparesheni na kupata kazi.Neno: Zab. 30:1-2. Wimbo: Zawadi gani (Kwaya ya Vijana).
 1. Fellowship leo itakuwepo kuanzia saa 9.00 alasiri. Aidha Alhamisi ijayo tarehe 10.11.2016 saa 11.00 jioni kutakuwa na maombi na maombezi yatakayoongozwa na mtumishi Sweetbert Lugemalila.  Wagonjwa na wenye shida mbalimbali pia watapata huduma siku hiyo. Wote mnakaribishwa na muwaarifu na wengine.
 1. Vikundi vyote vya usharika mnaombwa kuwasilisha bajeti ya kikundi kwa mwaka 2017 katika ofisi ya wahasibu kabla ya tarehe 17.11.2016.

 

 1. NDOA:

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 19.11.2016

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Ronald Justo Mbowe          na     Bi. Upendo Gilliaara Nkini

Ndoa ifuatayo itafungwa Katoriki Parokia ya Tagaste Chekereni Parish kati ya

Bw. Joachim Heven Meena       na     Bi. Prisca Said

 

TAREHE 20.11.2016

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Erick Rwemanya Lutahakana      na     Bi. Hellen Fredrick Fungamtama

 

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 12.11.2016

SAA 10.00 JIONI

Bw. Eric Siddon Mosha             na     Bi. Akarii Abdallah Godigodi

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga: Watatangaziana
 • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bibi Mary Mungure
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watatangaziana
 • Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
 • Tabata: Watatangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Watatangaziana
 • Mjini kati: Watatangaziana
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:  Kwa Bwana na Bibi Moshi

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki