MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 04 FEBRUARI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI NENO LA MUNGU LINA NGUVU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Leo kutakuwa na felloship hapa Usharikani kuanzia saa 9.00 alasiri. Washarika wote mnakaribishwa. Aidha kipindi cha maombi na maombezi  kitafanyika  Alhamisi ijayo tarehe 08-02-2018 saa 11:30 jioni. Tunapenda kuwahimiza washarika kuhudhuria kwa wingi.

4. Leo tutamtolea Mungu Fungu la kumi.  Washarika karibuni

5. Jumapili ijayo tarehe 11/02/2018 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini.  Atakayehitaji huduma hii afike ofisini kwa Mchungaji.

6. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwakumbusha Washarika wote waliochukua bahasha kwa ajili ya kuchangia ada za watoto wa kituo cha Don Bosco waziridishe kwa Parish Worker au kwa viongozi wa Umoja wa Wanawake, kwa wale waliokwisha rudisha bahasha hizo wafike ofisini kwa Parish Worker wachukue risiti zao.

7. Jumapili ijayo tarehe 11/02/2018 katika ibada ya kwanza saa 1.00 asubuhi, Kwaya ya Upendo watamshukuru Mungu kwa mema mengi aliyowatendea kwa mwaka uliopita wa 2017 na kuwaingiza tena salama katika mwaka huu wa 2018.

Neno: Zaburi 133,  Wimbo: Kama si wewe – toka Kwaya ya Upendo.

8. Tunapenda kuwatangazia washarika wanaotaka kufunga ndoa wajiandikishe mapema miezi mitatu kabla au zaidi.  Ndoa za Mwezi April, Mei, Juni na Julai Mafundisho Kidayosisi yatafanyika tarehe 10/03/2018 na 17/03/2018 Jumamosi saa 3.00 asubuhi katika Usharika wa Magomeni Mviringo. Ratiba yote imebandikwa kwenye ubao wa Matangazo Karibu na duka letu la Vitabu.

9. Jumanne ijayo tarehe 06/02/2018 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Baraza la Wazee.  Wajumbe wote mnakumbushwa  kuhudhuria kikao hiki muhimu.

10. Kwaya Kuu ya Usharika itasafiri alhamisi ijayo tarehe 08/02/2018 kwenda Kanisa Kuu Dodoma hadi tarehe 11/02/2018.  Washarika tuwaombee.

11. Jumatano ya tarehe 14/02/2018 itakuwa ni siku ya majivu hivyo Jumuiya zote mnakumbushwa kujiandaa kwa ajili ya kuongoza ibada za kila Jumatano ya Majivu.  Ratiba kamili itatolewa.

12. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 10/02/2018

Bwana Gustav Bapas Mphusu                 na     Rose Juma Tang’are

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

12. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Hillary Mushi
  • Kinondoni: Kwa Profesa Geofrey Mmari
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Itemba
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Mollel David Mollel
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Sangiwa
  • Mjini kati:  Kwa Mama Lyidia Ngwale
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Dr. Abed na Eng. Elisifa Kinasha