MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 04 DESEMBA, 2016

NENO LINALOTUONGOZA  NI BWANA ANAKUJA KATIKA UFALME WAKE

 

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

 

 1. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia na Cheti:

 

 1. Leo tutamtolea Mungu fungu la kumi.

 

 1. Fellowship leo itakuwepo kuanzia saa 9.00 alasiri. Aidha kila  alhamisi ijayo tarehe 01.12.2016 saa 11.00 jioni kutakuwa na maombi na maombezi yatakayoongozwa na mtumishi Sweetbert Lugemalila. Wagonjwa na wenye shida mbalimbali watapata huduma siku hiyo. Wote mnakaribishwa sana.

 

 1. Jumamosi  ijayo tarehe 10/12/2016 saa 4.00 asubuhi kutakuwa na kikao cha Wajane na Wagane. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria.
 2. Leo baada ya ibada ya pili kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Vijana hapa Usharikani katika ukumbi wa chini. Vijana wote mnaombwa kuhudhuria.
 1. Mkutano Mkuu wa 33 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani utafanyika tarehe 11-14 Desemba, 2016 Kisarawe Junior Seminary. Washarika tuendelee  kuuombea Mkutano huu.

 

 1. NDOA:

 

Matangazo ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu

 

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga: Kwa Simbo Nkya
 • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Edward Mkony
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watatangaziana
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watatangaziana
 • Oysterbay/Masaki: Jaji Mlay
 • Tabata: Watatangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Watatangaziana
 • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi S. Mkocha
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:  Watatangaziana

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki